Kwa nini mahakama ni muhimu
Mahakama hufasiri sheria, hutatua migogoro, na huhakikisha kila mtu — ikiwemo serikali — anafuata Katiba. Lazima ziwe huru na za haki.
Art. 159
(1) Mamlaka ya Mahakama yanatokana na watu, yanajikita katika mahakama na mahakama maalum zinazobuniwa kulingana na Katiba hii. (2) Katika kutekeleza majukumu ya kimahakama, mahakama na mahakama maalum zitaongozwa na kanuni zifuatazo- (a) haki itatendwa kwa kila mtu bila kuzingatia hadhi ; (b) Haki haitacheleweshwa; (c) njia m’badala za kusuluhisha kesi zikiwemo msamaha, mashauriano, na maridhiano na njia za kitamaduni za kusuluhisha migogoro zitaimarishwa, kwa mujibu wa ibara ya (3); (d) haki itatolewa kwa kuzingatia matatizo yaliyopo ya utaratibu wa kitaalamu; na (e) lengo na kanuni za Katiba hii zitatunzwa na kuendelezwa. (3) Mbinu za kitamaduni za utatuaji wa migogoro hazitatumiwa kwa njia ambayo- (a) itakiuka Sheria za Haki; (b) itagongana na haki na maadili au kusababisha matokeo yatakayogongana na haki na maadili; (c) haiambatani na Katiba hii au sheria yoyote iliyoandikwa.
Soma kifungu kamili →Art. 160
(1) Katika utekelezaji wa mamlaka ya mahakama, Mahakama kama ilivyoundwa chini ya kifungu cha 161, itazingatia Katiba hii pamoja na sheria na haitadhibitiwa wala kuelekezwa na mtu yeyote mwingine au halmashauri. (2) Afisi ya jaji wa mahakama ya Mamlaka Kuu haitafutiliwa mbali wakati ambapo kuna afisa anayeshikilia wadhifa huo. (3) Mishahara na marupurupu yanayofaa kulipwa, au kuhusiana na, majaji yatatoka kwa Mfuko wa Jumla wa Serikali. (4) Kulingana na Kifungu cha 168 (6), mishahara na marupurupu inayofaa kulipwa, au kuhusiana na majaji haitabadilishwa kwa njia itakayowaathiri, na marupurupu ya kustaafu ya jaji hayatabadilishwa ili kumuathiri jaji mstaafu katika maisha yake ya uhai. (5) Mwanachama wa mahakama hatawajibika katika hatua au kesi kuhusiana na chochote watakachofanya au watakachokosa kufanya kwa nia njema katika utendaji kazi wa kisheria kwa kutekeleza majukumu ya mahakama.
Soma kifungu kamili →