Ugatuzi ni nini?
Ugatuzi ni kugawana mamlaka kati ya serikali ya kitaifa na serikali 47 za kaunti, ili maamuzi yafanywe karibu na wananchi.
Art. 6
(1) Eneo la Kenya limegawanywa katika kaunti zilizotajwa katika Mpangilio wa Kwanza. (2) Serikali katika viwango vya kitaifa na kaunti ni tofauti na zinategemeana na Zitaendesha mahusiano yao ya uelewanaji kwa misingi ya mashauriano na ushirikiano. (3) Asasi ya Serikali ya kitaifa itahakikisha ufikiaji wa huduma zake bora katika sehemu zote za Jamhuri kwa njia inayofaa na kulingana na hali ya huduma inayotakikana
Soma kifungu kamili →Art. 174
Malengo ya Serikali ya ugatuzi ni- (a) kuhakikisha kuwa kuna mamlaka ya kidemokrasia na uwajibikiaji wa Serikali ; (b) kuhimiza umoja wa kitaifa kwa kutambua uanuwai wa jamii mbalimbali; (c) kuwapa watu katika kila ngazi mamlaka ya kujitawala na kushiriki katika matumizi ya mamlaka ya Serikali katika kufanya maamuzi ya mambo yanyowaathiri; (d) kutambua haki za jamii zote katika kusimamia masuala ya jamii zao na kujiendeleza zaidi; (e) kulinda na kuhamasisha maslahi na haki za jamii za watu walio wachache na zile za watu waliotengwa; (f) kustawisha miradi ya kijamii na kiuchumi na utoaji wa huduma za karibu na zilizo rahisi ili kumfikia kila mtu nchini Kenya; (g) kuhakikisha kuna ugavi sawa wa rasilmali zote za kijamii na za kitaifa kote nchini. (h) kufanikisha ugatuzi wa mamlaka ya taasisi za Serikali, uendeshaji wake wa shughuli ama huduma kutoka mji mkuu wa Kenya; na (i) kuhakikisha kuna kudhibiti na kugawana mamlaka kwa njia iliyo sawa.
Soma kifungu kamili →